Jamii za Kiislamu zinaitizama Majlisi kama hii kuwa ni fursa muhimu ya kufundisha na kuongeza ufahamu wa hadhira kuhusu historia na siasa za kanda, pamoja na kutoa mwongozo juu ya namna ya kuendeleza mshikamano wa kidini na kijamii katika nyakati za changamoto.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii tarehe 29-09-2025, katika Majlisi maalumu ya kumbukumbu ya kifo cha Kishahidi cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah, Sheikh Suleiman alihutubia hadhira akielezea kwa kina mgawanyo wa kisiasa na kijiografia wa nchi za Mashariki ya Kati. Sheikh Suleiman alisisitiza uwepo wa umuhimu wa kuelewa tofauti za kihistoria, kidini na kisiasa kati ya nchi za kanda hii ya Mashariki ya Kati ili kuimarisha mshikamano wa kikanda na upinzani dhidi ya vikwazo vya kigeni.
Majlisi hiyo ilihudhuriwa na wanajamii, wakiwemo viongozi wa kidini, Walimu na Wanafunzi wa elimu ya dini, pamoja na wanahabari wa vyombo vya habari vya kidini na vya kawaida. Sheikh Suleiman pia alisisitiza jukumu la vijana katika kudumisha kumbukumbu za Mashahidi na kuendeleza misimamo ya haki na usawa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Your Comment