Miongoni mwa Faida Kuu za Dua ya Tawasul kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu na mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s): Kumfanya mtu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu - kupitia kuwataja na kuwatawadha Ahlul-Bayt (a.s) kama njia ya ukaribu kwa Mola.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Leo hii (Jana Jumanne - 30 September 2025) Katika mazingira ya kiroho ya Madrasat ya Banati ya Sayyidat Zainab (SA) iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam - Tanzania, iliandaliwa kikao maalumu cha kuhuisha Usomaji wa Dua ya Tawasul. Kikao hiki cha kiibada kilihudhuriwa na Wanafunzi wote wa Madrasat hii ya Sayansi ya Ahlul-Bayt (as), kilichofanyoka mara tu baada ya Swala ya Magharibi na Isha, na kuendelea kwa muda wa dakika 35.
Qur’an Tukufu na maneno matukufu ya Dua ya Tawasul yaliosomwa kwa pamoja huku yakiujaza ukumbi wa Husseiniyyah kwa hali ya utulivu na unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu.
Washiriki wote walipata fursa ya kujiweka karibu na Ahlul-Bayt (a.s) kupitia maneno mazuri ya dua hiyo, na kuomba uongofu, baraka na mafanikio katika njia ya elimu na ucha Mungu.
Kikao hiki cha kiroho cha Dua ya Tawasul kimepokelewa na Wafuasi kwa moyo wa furaha na kushiriki kwa wingi, na kuwaacha wakiwa na hali ya faraja na msisimko wa kiroho.
Faida: Kuna Faida na Umuhimu wa Dua ya Tawasul katika Maisha ya Muislamu
Zifuata ni faida kuu za Dua ya Tawasul kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu na mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s):
- Kumfanya mtu kuwa karibu na Mwenyezi Mungu - kupitia kuwataja na kuwatawadha Ahlul-Bayt (a.s) kama njia ya ukaribu kwa Mola.
- Kujibiwa dua na haja - imepokewa kuwa mwenye kusoma Dua ya Tawasul kwa ikhlasi, haja zake hukaribia kutimizwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
- Kuzidisha imani na upendo kwa Ahlul-Bayt (a.s) - dua hii inasisitiza nafasi yao ya uombezi na cheo chao mbele ya Allah.
- Kutuliza moyo na kuondoa huzuni – kwa sababu ya maneno yake ya kiroho yanayojaza matumaini na msamaha.
- Kukuza mshikamano wa kijamii na kiroho - inaposomewa kwa pamoja, huleta hali ya mshikamano wa kiimani na kiroho miongoni mwa washiriki.
- Kufundisha adabu ya dua na tawasul - inamfunza muumini namna ya kuomba, kwa unyenyekevu na kupitia njia iliyokubalika na Mwenyezi Mungu.
Your Comment