Sheikh Jalala aliwahimiza Waumini wa Mkoa wa Geita kushikamana kwa dhati na mafundisho ya Uislamu sahihi unaofundishwa na Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na kizazi chake kitakasifu.

1 Oktoba 2025 - 12:04

Ziara ya Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (T.I.C) Kanda ya Ziwa +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA-Runzewe - Geita (30/09/2025): Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, ameendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa, akiwatembelea Waumini wa Runzewe, Mkoa wa Geita na kufanya Mkutano Maalum uliowahusisha Waumini wa eneo hilo. Katika mkutano huo wa kiroho, Sheikh Jalala aliwahimiza Waumini kushikamana kwa dhati na mafundisho ya Uislamu sahihi unaofundishwa na Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na kizazi chake kitakasifu.

Ziara ya Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (T.I.C) Kanda ya Ziwa +Picha

Katika nasaha zake, alisisitiza kuwa uongofu na mafanikio ya waumini yapo katika kushikamana na mafundisho haya, kwani ndiyo njia sahihi ya kuondoa mfarakano na kudumisha mshikamano wa kidini na kijamii.

Ziara ya Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (T.I.C) Kanda ya Ziwa +Picha

Mwanza (29/09/2025)
Katika sehemu nyingine ya ziara yake ya Kanda ya Ziwa, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, pamoja na jopo lake kutoka Dar es Salaam, walipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Deski and Chair, Ndugu Hajji Sibtwain, katika ofisi zake jijini Mwanza.

Sambamba na kikao hicho, Sheikh Jalala alimkabidhi Ndugu Sibtwain tuzo ya ardhi yenye ukubwa wa ekari saba, ambayo ilitolewa wakati wa sherehe za Maulid ya Mkoa wa Mwanza na kupokelewa kwa niaba ya mfadhili Nasser Virji. Ardhi hiyo imetolewa kwa lengo la ujenzi wa shule ya msingi Mbugani, jijini Mwanza, ili kusaidia juhudi za kuendeleza elimu kwa watoto wa eneo hilo.

Ziara ya Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (T.I.C) Kanda ya Ziwa +Picha

Kwa hatua hiyo, Sheikh Jalala alisisitiza umuhimu wa elimu bora kwa kizazi kipya, akibainisha kuwa taasisi za Kiislamu zinapaswa kushirikiana kwa karibu katika kuwekeza kwenye elimu, ambayo ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya jamii.

Your Comment

You are replying to: .
captcha