Sheikh Ja’far alisisitiza umuhimu wa kusoma Qur’an kwa sauti nzuri, kwa ufasaha, na kwa umakini mkubwa, jambo linalosaidia kuimarisha kumbukumbu, kuelewa maana, na kuongeza thamani ya maombi na ibada.

2 Oktoba 2025 - 12:36

Somo la Qur’an Tukufu katika Madrasat ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni , Dar-es-salaam +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Shule ya Mabinti wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (sa) wiki hii imeendelea na mfululizo wa masomo ya Qur’an Tukufu chini ya usimamizi wa Sheikh Mohammed Ja’far, mwalimu mahiri na mwenye uzoefu mkubwa katika ufundishaji wa Qur’an. Masomo haya yameandaliwa kwa malengo ya kukuza uelewa wa Qur’an, kuboresha matamshi sahihi, na kuimarisha adabu ya kusoma Kitabu Tukufu cha Mwenyezi Mungu.

Somo la Qur’an Tukufu katika Madrasat ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni , Dar-es-salaam +Picha

Somo hili lilidumu kwa muda wa saa moja na lilihudhuriwa na walimu wote pamoja na wanafunzi wa madrasat husika.Sheikh Ja’far aliwasilisha masomo kwa ufafanuzi wa kina, akizingatia kutadaburi Aya Tukufu za Qur’an, kuelezea hukumu zake, na kufundisha matamshi sahihi ya herufi za Qur’an.

Aidha, Sheikh Ja’far alisisitiza umuhimu wa kusoma Qur’an kwa sauti nzuri, kwa ufasaha, na kwa umakini mkubwa, jambo linalosaidia kuimarisha kumbukumbu, kuelewa maana, na kuongeza thamani ya maombi na ibada.

Shule ya Mabinti wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (sa) inaendelea kujitahidi kutoa mafundo bora ya Qur’an kwa wanafunzi wake, ikiwa ni sehemu ya malengo yake ya kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa ya dini yenye msingi thabiti, maadili mema, na uelewa wa Qur’an kwa kina.

Somo la Qur’an Tukufu katika Madrasat ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni , Dar-es-salaam +Picha

Mratibu wa program: Madrasat Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni.

Your Comment

You are replying to: .
captcha