Mufti alipokelewa na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Katibu wa Mkoa, pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkoa wa Dodoma, wakiwa wameambatana na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWAT).

7 Oktoba 2025 - 14:24

Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zuberi, amewasili leo tarehe 7 Oktoba 2025 Jijini Dodoma, kwa ajili ya kuanza Ziara ya Kichungaji na Kidaawa katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikiwemo Iringa, Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Mufti Awasili Dodoma Tayari kwa Ziara za Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini +Picha

Katika mapokezi hayo, Mufti alipokelewa na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Katibu wa Mkoa, pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkoa wa Dodoma, wakiwa wameambatana na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Mufti Awasili Dodoma Tayari kwa Ziara za Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini +Picha

Ziara hiyo inatarajiwa kujikita katika kuimarisha shughuli za dini, kuhimiza umoja wa Waislamu, na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili viongozi wa mikoa na wilaya katika utekelezaji wa majukumu yao ya kiimani na kijamii. 

Mufti Awasili Dodoma Tayari kwa Ziara za Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha