Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) limewapongeza wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) Tanzania kwa mafanikio yao na mchango wao katika kukuza elimu na tafiti bunifu nchini Tanzania.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Mashindano ya Kisayansi na Kimaarifa yalifanyika Kibaha, Jumapili tarehe 12 Oktoba 2025, yakihusisha wanafunzi kutoka taasisi mbalimbali za kidini na kisekula. Mashindano hayo yalijikita katika mada kadhaa za utafiti wa kisayansi na Kimaarifa, zikiwemo tafiti kuhusu uchawi kwa mujibu wa Qur’an na Sunna, uchambuzi wa Aya za Qur’an, na mchango wa elimu ya dini katika kupunguza imani za kishirikina.
Miongoni mwa washiriki ni Chuo cha Al-Mustafa (s) Tanzania, ambapo wanafunzi wavulana wa Chuo hicho cha Al-Mustafa - Mbezi Beach walionyesha umahiri mkubwa katika Mashindano hayo, na hatimaye wakaibuka washindi wa nafasi ya pili.
Ushindi huo umetajwa kuwa ishara ya ubunifu, juhudi, na umahiri wa wanafunzi wa Al-Mustafa (s) katika nyanja za utafiti wa kisayansi, kijamii na kielimu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) limewapongeza wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) Tanzania kwa mafanikio yao na mchango wao katika kukuza elimu na tafiti bunifu nchini Tanzania.
Your Comment