Sheikh Mustafa Shirazi: "Mwenyezi Mungu husaidia wale wanaojisaidia wenyewe, hivyo mnapaswa kuwa na nia safi, jitihada za kweli, na tumaini kwa Allah katika kila hatua ya elimu yenu".

24 Oktoba 2025 - 18:18

Bilal Muslim Mission - Kagera yafanya Dua Maalum kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwabuki - Bukoba + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Kagera, Bukoba - Tarehe 18 Oktoba 2025 - Uongozi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania - Kagera umehudhuria dua maalum iliyofanyika kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwabuki - Bukoba, ambao wako katika maandalizi ya mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Pili.

Msafara huo wa dua ulianzia katika Hauzatu AhlulBayt - Hamugembe, ukiongozwa na Alhaj Muhammad Manji, Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission – Kagera, akiwa ameambatana na Sheikh Mustafa Shirazi, Mudiri wa Hauza, pamoja na viongozi wengine wa AhlulBayt Hamugembe, Bukoba Mjini.

Katika hafla hiyo yenye mazingira ya kiroho na ushirikiano, viongozi hao walitoa nasaha kwa wanafunzi, wakisisitiza umuhimu wa kutegemea Mwenyezi Mungu (s.w.t), kuwa na bidii katika masomo, na kudumisha maadili mema ndani na nje ya shule.

Bilal Muslim Mission - Kagera yafanya Dua Maalum kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwabuki - Bukoba + Picha

Sheikh Mustafa Shirazi aliwakumbusha wanafunzi kwamba elimu ni amana na nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ni wajibu kwa kila mwanafunzi kuitumia kwa njia sahihi kwa manufaa ya jamii. Aliongeza kuwa dua na juhudi vinapaswa kwenda sambamba, akisema:

“Mwenyezi Mungu husaidia wale wanaojisaidia wenyewe, hivyo mnapaswa kuwa na nia safi, jitihada za kweli, na tumaini kwa Allah katika kila hatua ya elimu yenu.”

Kwa upande wake, Alhaj Muhammad Manji alitoa pongezi kwa walimu na uongozi wa shule kwa malezi mema wanayowapa wanafunzi, akiahidi kuwa Bilal Muslim Mission - Kagera itaendelea kuwa bega kwa bega na taasisi za elimu katika kuwalea vijana kiimani na kimaadili.

Wanafunzi walionyesha furaha na shukrani zao kwa ugeni huo, huku wakiomba dua kwa Mwenyezi Mungu awape wepesi, maarifa, na mafanikio katika mitihani yao ijayo.

Bilal Muslim Mission - Kagera yafanya Dua Maalum kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwabuki - Bukoba + Picha

Tunatoa shukrani za dhati kwa Alhaj Muhammad Manji kwa kujitolea kuongoza safari hii ya kiroho na kuonesha mfano wa uongozi wa karibu na jamii.

“Mwenyezi Mungu (s.w.t) awape wanafunzi wote wepesi, utulivu wa moyo, na mafanikio mema katika mitihani yao na maisha yao kwa ujumla.”

Bilal Muslim Mission - Kagera yafanya Dua Maalum kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwabuki - Bukoba + Picha

Imeandaliwa na:
Harakati ya Tabligh – Hauzatu AhlulBayt (a.s), Hamugembe, Bukoba Mjini.

Your Comment

You are replying to: .
captcha