Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Mwenyezi Mungu (SWT) anasema: “Na vazi la uchamungu ndilo bora zaidi; hayo ni katika alama za Mwenyezi Mungu ili mpate kukumbuka.” ﴿ يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ﴾ (Surat Al-A‘rāf, 7:26) Leo, (Jumatatu) tarehe 20 Oktoba 2025, katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Khidr Kano amevikwa rasmi taji la kielimu (Rawani) katika hafla iliyoongozwa na Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Kiislamu Sayyid Ali Al-Khamenei (Q.S) barani Afrika, Sheikh Mahdawy. Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo alikuwa Sheikh Yakub Yahya Katsina, ambaye alitoa pongezi kwa Sayyid Khidr kwa kupata heshima hiyo kubwa, na akamtakia mafanikio mema katika kuutumikia Uislamu na Umma wa Mtume (s.a.w.w). Katika hotuba yake fupi kwa lugha ya Kiarabu, Sheikh Yakub alisisitiza kuwa rawani huo uwe alama ya uchamungu na utiifu kwa Mwenyezi Mungu, akirejea maneno ya Qur’ani yanayokumbusha kwamba vazi bora ni “vazi la taqwa.” Hafla hiyo ilipambwa na uwepo wa wanazuoni na wanafunzi wa elimu za dini, na picha kadhaa zilipigwa kukumbusha tukio hilo muhimu.

Your Comment