Kwa mujibu wa taarifa kutoka uongozi wa Hawza, mtihani huo ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo katika kuimarisha elimu ya Kiislamu yenye mizizi ya Qur’an Tukufu na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Ahlul Bayt wake (a.s).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam – Hawza ya Imam Ridha (a.s), chini ya usimamizi wa Taasisi ya Kiislamu ya: Hujjatul Asr Society of Tanzania, chini ya Kiongozi wake Mkuu Sayyid Arif Naqvi, Leo hii tarehe 08-11-2925 imeendesha mtihani wa mwisho wa mwaka wa 2025 katika katika Maarifa ya Kiislamu, kwa kushirikisha wanafunzi wa elimu ya Dini katika tawi la Ikwiriri – Rufiji, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka uongozi wa Hawza, mtihani huo ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo katika kuimarisha elimu ya Kiislamu yenye mizizi ya Qur’an Tukufu na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Ahlul Bayt wake (a.s).
Akizungumza katika muktadha huo, Mwalimu Mkuu wa Hawza, Sheikh Idi Harun, alisema kuwa lengo la mtihani huu ni kupima kiwango cha uelewa wa Wanafunzi na kuwahamasisha kuendeleza elimu ya Dini kwa misingi ya utafiti na uadilifu.
“Tunataka kuona Wanafunzi wetu wakijenga msingi imara wa elimu ya Kiislamu, unaochanganya maarifa ya kielimu na maadili mema. Hawza ya Imam Ridha (a.s) inapania kuandaa kizazi cha viongozi wa Kiislamu wenye hekima, imani na maarifa ya kina,” alisema Sheikh Idi Harun.
Matokeo ya mtihani huu yanatarajiwa kutangazwa mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa usahihishaji na tathmini ya kitaaluma, chini ya uangalizi wa walimu na idara ya elimu ya Dini katika Hawza husika.
Your Comment