Kwa ujumla, mitihani ya leo imeendeshwa kwa mafanikio makubwa. Waalimu wameeleza kuridhika kwao na juhudi za wanafunzi, huku wakitarajia matokeo mazuri yatakayoendana na bidii waliyoionyesha wakati wa maandalizi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo, Tarehe 18/11/2025 katika Hawzah ya Imam Zaynul Aabidin (a.s), mitihani ya mwisho wa muhula wa pili -2025 imefanyika kwa utulivu mkubwa na mpangilio mzuri. Wanafunzi wamejitokeza kwa ari na umakini, wakionyesha maandalizi mazuri na nidhamu katika kushiriki mitihani yao.

Walimu na wasimamizi pia walikuwepo kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa ipasavyo na mazingira yanabaki kuwa rafiki kwa wanafunzi.
Masomo yaliyofanyiwa mtihani leo ni haya yafuatayo:
1_Hifdhi ya Qur’an Tukufu
2_Tafsiri (al-Tamhīdī)
3_Kitabu cha Manīyat al-Murīd
4-Masadir za Sunna Tukufu
5-Somo la Kompyuta (mbinu na msingi wa uendeshaji).
N.k

Kwa ujumla, mitihani ya leo imeendeshwa kwa mafanikio makubwa. Waalimu wameeleza kuridhika kwao na juhudi za wanafunzi, huku wakitarajia matokeo mazuri yatakayoendana na bidii waliyoionyesha wakati wa maandalizi.

Uongozi wa shule unawaombea wanafunzi wote mafanikio mema katika mitihani yao, pamoja na kuwatakia neema na baraka katika safari yao ya elimu na malezi ya kiakhlaki.
Your Comment