Shirika la Habari la Kimatafa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kikao maalumu cha kujadili mitazamo na fikra zinazofanana kuhusu turathi za Basra kimefanyika leo asubuhi, Jumanne (25-11-2025), kwa ushiriki wa wakurugenzi kutoka Idara ya Masuala ya Maarifa ya Kiislamu na Kibinadamu ya Ataba ya Abbasiyya, wakurugenzi wa Kituo cha Turathi za Basra, pamoja na viongozi wa vituo vya utafiti vya kielimu kutoka vyuo vikuu na Hawza. Kikao hiki, ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Ataba ya Abbasiyya, Kituo cha Turathi za Basra, na idadi ya taasisi za kielimu za Hawza na Chuo Kikuu cha Qom, kimefanyika katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa Kituo cha Fiqhi cha Maimamu Watoharifu (a.s.) mjini Qom.
26 Novemba 2025 - 23:25
News ID: 1754573

Your Comment