Allah aendelee kutujaalia kufuata nuru ya Ahlul-Bayt (a.s).

13 Desemba 2025 - 12:50

Sherehe za Maulid ya Bibi Mtukufu Fatima binti wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) zilifana kwa kiwango kikubwa mjini Nakuru mwaka 2025

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Nakuru | 2025 Waumini kutoka maeneo mbalimbali walihudhuria kwa wingi kushiriki katika kumbukumbu hii tukufu, iliyojaa mawaidha, qasida, dua na hotuba za kielimu zilizoangazia fadhila, nafasi na mchango wa Sayyidat Fatima Zahra (a.s) katika Uislamu.

Masheikh na wanazuoni walisisitiza:

1_Nafasi ya Fatima (a.s) kama kigezo cha mwanamke mwema na mama wa Umma

2_Uhusiano wake wa karibu na Mtume (s.a.w.w) na kauli zake mashuhuri kuhusu yeye

3_Umuhimu wa kufuata mwenendo wake katika ibada, maadili, subira na ulinzi wa haki.

Sherehe hizi ziliimarisha:

1_Umoja wa Waumini,

2_Mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s),

3_Uelewa wa kielimu na kiroho, hususan kwa vijana.

Kwa hakika, Maulid hii ilikuwa tukio la kihistoria na lenye baraka, lililoacha athari chanya katika jamii ya Kiislamu ya Nakuru.

Allah aendelee kutujaalia kufuata nuru ya Ahlul-Bayt (a.s).

Sherehe za Maulid ya Bibi Mtukufu Fatima binti wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) zilifana kwa kiwango kikubwa mjini Nakuru mwaka 2025

Your Comment

You are replying to: .
captcha