Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-; Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nchini Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky (Allah Amhifadhi) ametembelea Haram ya Imam Khomeini (RA) Siku ya Jumanne katika Jiji la Tehran. Katika ziara hiyo, Sheikh Zakzaky (M.A) alitoa heshima zake katika Haram ya Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Ruhollah Khomeini (RA), huku akitafakari urithi wake wa mapambano, uadilifu na kusimamia haki za wanyonge. Ziara hiyo inaashiria mshikamano wa kifikra na kiroho pamoja na kuthamini mchango wa Imam Khomeini (RA) katika historia ya Uislamu na harakati za Kiislamu duniani.

17 Desemba 2025 - 15:12

Your Comment

You are replying to: .
captcha