Tunamuomba Mwenyezi Mungu azikubali ibada za Masheikh wetu, awajaalie Umrah yao iwe Umrah yenye kukubalika (Umrah Maqbulah), na arejeshe thawabu zake kwa Ummah wote wa Kiislamu.

24 Desemba 2025 - 13:34

Faida na Thawabu za Kufanya Umrah Mufradah kwa Mujibu wa Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa uwezo wa Allah (SWT) - Baada ya Masheikh wetu - Allah awatakabalie Amali zao - kuvaa Ihram katika Msikiti wa Shajara (Masjid al-Shajarah) uliopo Madinatul-Munawwara, sasa wameanza safari ya kiroho kuelekea Mji Mtukufu wa Makka kwa lengo la kutekeleza Manasik za Umrah Mufradah.

Hatua hii ni ishara ya kuingia katika hali ya utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu na kujitenga na masuala ya kidunia, kwa kufuata sunnah na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) pamoja na Ahlul-Bayt wake watukufu (a.s.).

Faida na Thawabu za Kufanya Umrah Mufradah kwa Mujibu wa Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) +Picha


Kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), Umrah Mufradah si ibada ya kawaida tu, bali ni ibada yenye fadhila kubwa na athari ya kina katika maisha ya kiroho ya muumini.

Faida na Thawabu za Kufanya Umrah Mufradah kwa Mujibu wa Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) +Picha

Zifuatazo ni Fadhila na athari za kina za Ibada hii ya Umrah Mufradah katika maisha ya kiroho ya muumini:
1. Msamaha wa Dhambi na Utakaso wa Nafsi
Imepokewa kutoka kwa Imam Ja‘far al-Sadiq (a.s.) kwamba: “Kufanya Umrah huondoa umaskini na husafisha dhambi kama moto unavyosafisha chuma.”
Umrah Mufradah humrejesha muumini katika hali ya usafi wa kiroho, humfanya aanze ukurasa mpya wa maisha kwa toba ya kweli na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.


2Kuimarika kwa Imani na Ucha-Mungu (Taqwa)
Ihram humfundisha muumini unyenyekevu, usawa na nidhamu. Kuvaa vazi moja bila tofauti za hadhi au cheo huimarisha hisia ya usawa mbele ya Allah, jambo linalosisitizwa sana katika mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.).


3. Kuimarisha Uhusiano na Ahlul-Bayt (a.s.)
Umrah huambatana na ziyara ya Nyumba Tukufu ya Allah pamoja na dua na sala zinazopendekezwa na Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.). Ibada hii humfanya muumini awe karibu zaidi na misingi ya Wilayah na utiifu kwa viongozi wa haki.

Faida na Thawabu za Kufanya Umrah Mufradah kwa Mujibu wa Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) +Picha


4. Thawabu Kubwa na Fadhila Maalumu
Imepokewa kutoka kwa Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s.) kwamba: “Mtu anayefanya Umrah akiwa na ikhlasi hupata thawabu sawa na aliyefanya Jihad katika njia ya Allah.” Hii inaonyesha uzito na nafasi ya Umrah Mufradah katika mizani ya thawabu mbele ya Mwenyezi Mungu.


5. Kuondolewa kwa Dhiki na Kuongezeka kwa Riziki
Kwa mujibu wa riwaya nyingi za Ahlul-Bayt (a.s.), kufanya Umrah mara kwa mara huondoa dhiki, huzuni na matatizo ya maisha, na hufungua milango ya riziki halali na baraka.


6. Mafunzo ya Subira, Nidhamu na Maadili ya Kiislamu
Kutekeleza Manasik ya Umrah humfundisha muumini subira, udhibiti wa nafsi, kuheshimu wengine, na kuacha tabia zisizofaa, jambo linalochangia mabadiliko chanya ya kitabia hata baada ya kurejea nyumbani.

Kwa ujumla:
Umrah Mufradah, kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s), ni safari ya marejeo kwa Mwenyezi Mungu, utakaso wa nafsi na uimarishaji wa uhusiano wa muumini na Muumba wake. Ni ibada inayobeba fadhila za kidunia na akhera, na athari zake hudumu katika mwenendo wa maisha ya kila siku ya muumini.

Faida na Thawabu za Kufanya Umrah Mufradah kwa Mujibu wa Mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s) +Picha

Tunamuomba Mwenyezi Mungu azikubali ibada za Masheikh wetu, awajaalie Umrah yao iwe Umrah yenye kukubalika (Umrah Maqbulah), na arejeshe thawabu zake kwa Ummah wote wa Kiislamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha