Wananchi wa Iran wamefanya maandamano ya amani kote nchini kuadhimisha Dey 9, wakionyesha mshikamano wa kitaifa na uungaji mkono wao kwa serikali ya Kiislamu chini ya uongozi wa Ayatollah Ali Khamenei, huku wakikataa propaganda na njama za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu.

2 Januari 2026 - 23:55

Maandamano ya Kitaifa Iran: Wananchi Waonesha Uzalendo na Kuiunga Mkono Serikali ya Kiislamu +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamejitokeza kwa wingi katika miji mbalimbali kote nchini kushiriki maandamano ya amani, wakionyesha mshikamano wao na uungaji mkono thabiti kwa serikali yao chini ya uongozi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei.

Maandamano hayo yamefanyika katika muktadha wa kuadhimisha tukio la kihistoria la Dey 9, siku inayobeba maana kubwa katika historia ya kisiasa ya Iran, ambapo wananchi huonesha upya utii wao kwa misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kukataa kwao njama na propaganda za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu.

Washiriki wa maandamano hayo wamebeba mabango na kutoa kauli zinazoonesha msimamo wao wa pamoja dhidi ya juhudi za nje zinazolenga kuingilia masuala ya ndani ya Iran, kusambaza taarifa potofu na kuchochea fujo, ghasia na mifarakano ya kijamii kupitia makundi na vibaraka wao.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, ushiriki mpana wa wananchi katika maandamano haya unaakisi kiwango cha juu cha uzalendo wa Wairani na mshikamano wao wa kitaifa, sambamba na msimamo wao wa kutokuruhusu adui yeyote kuathiri usalama, uthabiti na mustakabali wa nchi yao.

Kwa ujumla, maandamano ya Dey 9 yamekuwa ujumbe wa wazi kwa dunia kwamba wananchi wa Iran wanaendelea kusimama bega kwa bega na serikali yao ya Kiislamu, wakilinda mamlaka ya kitaifa na maadili ya Mapinduzi ya Kiislamu, huku wakisisitiza kuwa Iran itaendelea kusonga mbele kwa umoja, uthabiti na kujitegemea licha ya shinikizo na njama za nje.

Maandamano ya Kitaifa Iran: Wananchi Waonesha Uzalendo na Kuiunga Mkono Serikali ya Kiislamu +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha