Kituo cha Masomo kwa Wanafunzi Afrika katika Atabat Al-Abbasiya kimeandaa hafla ya hitimisho la Qur’anil Tukufu katika Mwezi wa Ramadhan, ikiwaleta pamoja wanafunzi ili kuadhimisha Kikamilifu Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan kupitia kuisoma Qur’ani na kushiriki katika tafakari za kiroho na mafunzo ya Ramadan.

22 Februari 2026 - 23:09

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt(as) -ABNA- Kituo cha Masomo kwa Wanafunzi wa Bara la Afrika katika Atabat Al-Abbasiya kimeandaa hafla Maalum ya Kuhitimisha Qur’an Tukufu ndani ya Ramadan, ikiwaleta pamoja wanafunzi kutoka asili mbalimbali kuadhimisha Ramadhan Kareem kikamilifu.

Tukio hili limejumuisha kusomwa kwa Aya za Qur’an Tukufu, tafakari za kiroho, na mijadala juu ya umuhimu wa Ramadan katika kukuza imani, nidhamu, na mshikamano wa kijamii. Wanafunzi walishiriki kikamilifu katika kusoma Qur’ani, kushiriki mawazo yao, na kuonyesha shukrani zao kwa mwongozo na mafundisho ya Qur’ani, jambo lililofanya Hafla hii kuwa tajiri kiroho na yenye kusisimua kwa wote waliohudhuria.

Your Comment

You are replying to: .
captcha