Dkt.Taqavi, Mkurugenzi na Mwakilishi wa Jamiat al-Mustafa (s.a.w.w) nchini Tanzania, amehutubia Majlisi ya Maombolezo ya Imam Hussein (a.s.) katika Shule ya Hazrat Zaynab (s.a), akizungumzia Mapinduzi ya Karbala pamoja na kutoa maelekezo ya kielimu, kitamaduni na kiutafiti.

21 Juni 2026 - 15:18

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi ya maombolezo ya Imam Husayn ibn Ali imefanyika katika Shule ya Hazrat Zaynab (a.s.) nchini Tanzania, kwa ushiriki wa wanafunzi, walimu na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.).

Muhadhara mkuu ulitolewa na Hujjatul-Islam wal-muslimin Dkt. Ali Taqavi, Mkurugenzi na Mwakilishi wa Jamiat al-Mustafa (s.) nchini Tanzania, ambaye alifafanua malengo na misingi ya Mapinduzi ya Imam Hussein (a.s.). Alieleza kuwa harakati za Karbala zilikuwa ni mwamko wa kulinda Uislamu halisi, kupinga dhulma na ufisadi, na kuimarisha misingi ya haki, uadilifu na heshima ya mwanadamu.

Mbali na mada hiyo, Dkt. Taqavi alitoa maelekezo kuhusu masuala ya elimu, utamaduni na utafiti, akiwataka wanafunzi na walimu kuongeza juhudi katika kujifunza, kufanya tafiti zenye manufaa kwa jamii, na kuendeleza maadili ya Kiislamu pamoja na utamaduni wa Ahlul-Bayt (a.s.) katika shughuli zao za kila siku.

Majlisi hiyo ilihitimishwa kwa maombolezo na dua za kuwaombea mashahidi wa Karbala, huku washiriki wakihimizwa kuendelea kuenzi na kuhuisha ujumbe wa Imam Husayn ibn Ali kwa vitendo vya haki, subira na kujitolea kuitumikia dini na jamii.

Your Comment

You are replying to: .
captcha