Waislamu wa madhehebu ya Shia jijini Moshi wameendelea kufanya Majalisi za maombolezo ya Imam Hussein (a.s) katika Mwezi Mtukufu wa Muharram 1448H/2026, wakikumbuka shahada ya mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mashujaa wa Karbala waliopigania haki na uadilifu.

25 Juni 2026 - 23:28

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA–, Waislamu wa madhehebu ya Shia katika jiji la Moshi wameendelea na Majalisi za kumuomboleza Imam Hussein (a.s) katika Mwezi Mtukufu wa Muharram 1448H/2026.
 
Kwa mujibu wa picha kutoka katika shughuli hiyo, waumini walikusanyika kwa wingi kwa ajili ya kukumbuka shahada ya mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s), pamoja na mashujaa wa Karbala waliotoa maisha yao kwa ajili ya kutetea haki, uadilifu na kupinga dhulma.
 
Akihutubia katika Majlis hiyo, Khatibu **Sheikh Miraj Salim** alieleza kuwa tukio la Karbala ni somo la milele linalowafundisha Waislamu na wanadamu wote umuhimu wa kusimama katika upande wa haki, kujitolea kwa ajili ya maadili mema na kutokubali dhulma katika jamii.
 
Washiriki wa Majlis hiyo walisisitiza kuwa maadhimisho ya Muharram yana lengo la kuhuisha mafundisho ya Imam Hussein (a.s) na kuendeleza ujumbe wake wa uhuru, uadilifu na heshima ya utu wa binadamu.
 
Majalisi za Muharram zinaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, zikikusanya waumini kwa ajili ya maombolezo, mawaidha na kutafakari mafunzo ya tukio la Karbala.
 

Your Comment

You are replying to: .
captcha