Waumini wa Arusha wamefanya matembezi ya Amani ya Kidini kuhuisha kumbukumbu ya Imam Hussein (AS), yakianzia Husseiniya ya Imam Ridha (AS) Ngarenaro hadi Shamsi na kurejea Husseiniya, wakisisitiza kauli ya “Labbayka Ya Hussein” kwa ushiriki wa Taasisi ya Sayyid al-Shohadaa na jumuiya mbalimbali.

27 Juni 2026 - 12:17

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Waumini wa Kiislamu, Wapenzi na Mashia Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as),  sambamba na vijana wa Jumuiya mbalimbali, wamefanya matembezi maalum ya kidini katika Jiji la Arusha, ikiwa ni sehemu ya kuhuisha na kuenzi tukio la Karbala kwa kauli ya ushindi na utii “Labbayka Ya Hussein”.
 
Matembezi hayo yaliyoratibiwa na Taasisi ya Seyyid Shohadaa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Answer Imamia pamoja na vijana wa Tamsiya na Waislamu kwa ujumla, yamehusisha makundi mbalimbali ya waumini walioungana katika kuonesha mapenzi kwa Imam Hussein (AS).
 
Kwa mujibu wa taarifa, maandamano hayo yalianzia katika Husseiniya ya Imam Ridha (AS) iliyopo eneo la Ngarenaro, kisha kuelekea eneo la Shamsi, na baadaye kurejea katika Husseiniya, huku washiriki wakiimba kauli ya “Labbayka Ya Hussein” kwa ari na mshikamano mkubwa.
 
Viongozi wa shughuli hiyo wameeleza kuwa matembezi hayo ni sehemu ya kuhuisha ujumbe wa Karbala, unaosisitiza uadilifu, mapambano dhidi ya dhulma na kuimarisha mshikamano wa Kiislamu miongoni mwa waumini.
 
Shughuli hiyo imehitimishwa kwa maombi na dua maalum za kuenzi mashahidi wa Karbala na kuendeleza ujumbe wa Imam Hussein (AS) katika maisha ya kila siku ya Waislamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha