Wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaosoma nchini Iraq wamekutana na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), Ayatollah Reza Ramezani, ambapo walijadili njia za kuimarisha shughuli za tablighi na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) katika Bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaosoma katika taasisi za elimu ya juu nchini Iraq wamekutana leo mjini Karbala na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s.), Ayatullah Reza Ramezani.
Katika kikao hicho, pande hizo zilijadili masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za tablighi na kueneza mafundisho ya Uislamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) katika nchi za Afrika, pamoja na namna ya kuimarisha nafasi ya wahitimu wa vyuo vya kidini katika kuhudumia jamii zao baada ya kurejea makwao.

Washiriki wa mkutano walisisitiza umuhimu wa mshikamano, ushirikiano na kubadilishana uzoefu miongoni mwa wanafunzi wa Afrika, ili kuongeza ufanisi wa kazi za kielimu, kitamaduni na kidaawa katika bara hilo.
Kwa upande wake, Ayatullah Reza Ramezani alieleza umuhimu wa kuwaandaa wanafunzi kielimu, kiakhlaqi na kifikra ili wawe mabalozi bora wa mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.), wenye uwezo wa kujibu changamoto za jamii na kueneza ujumbe wa Uislamu kwa hekima, busara na mazungumzo yenye kujenga umoja.

Maoni yako