Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania (T.I.C) imeandaa zafa maalumu ya kusherehekea Maulidi ya Mtume Muhammad (saww), iliyofanyika tarehe 30 Agosti 2026 katika eneo la Kigogo Post, Dar es Salaam, chini ya kaulimbiu ya “Amani, Upendo na Huruma” ikiwa ni miongoni mwa mafundisho muhimu ya Mtume Muhammad (saww).

1 Septemba 2026 - 19:41

T.I.C Yaandaa Zafa la Maulidi ya Mtume Muhammad (saww) Kigogo Post: “Amani, Upendo na Huruma Ndiyo Mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)” +Picha

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania (T.I.C) imefanya zafa maalumu kwa ajili ya kusherehekea Maulidi ya Mtume Muhammad (saww), katika hafla iliyofanyika tarehe 30 Agosti 2026, Kigogo Post, Dar es Salaam.

Zafa hiyo ilifanyika katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saww), huku waumini wakishiriki katika shughuli mbalimbali za kumuenzi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na kukumbushana mafundisho yake muhimu.

Kaulimbiu ya zafa hiyo ilikuwa “Amani, Upendo na Huruma”, ikisisitiza umuhimu wa kuhuisha mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) katika jamii, hususan katika kujenga amani, kuimarisha upendo na kueneza huruma miongoni mwa watu.

T.I.C Yaandaa Zafa la Maulidi ya Mtume Muhammad (saww) Kigogo Post: “Amani, Upendo na Huruma Ndiyo Mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)” +Picha

Maulidi hayo pia yalitoa fursa kwa washiriki kukumbushana kwamba mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) yanahimiza umoja, mshikamano, kuheshimiana na kuishi kwa amani, hivyo jamii inapaswa kuyatekeleza katika maisha ya kila siku.

Hafla hiyo ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika nchini Tanzania katika kuadhimisha Maulidi ya Mtume Muhammad (saww) na kuhuisha mafundisho na mwenendo wake katika jamii.

T.I.C Yaandaa Zafa la Maulidi ya Mtume Muhammad (saww) Kigogo Post: “Amani, Upendo na Huruma Ndiyo Mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)” +Picha

Maoni yako

You are replying to: .
captcha