Main Title

source : Parstoday
Jumanne

15 Novemba 2022

16:45:29
1323364

Wanamuqawama watekeleza oparesheni huko Ukingo wa Magharibi; Wazayuni 2 waangamizwa

Duru za habari zimeripoti kuwa, wanamuqawama wa Palestina wametekeleza oparesheni dhidi ya Uzayuni karibu na kitongoji kimoja cha walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharonot limetangaza leo Jumanne kwamba, walowezi wawili wa Kizayuni wameangamizwa na wengine watatu wamejeruhiwa katika oparesheni ya kimuqawama iliyofanywa na kijana Mpalestina karibu na kitongoji cha Ariel huko Silfit katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.   

Oparesheni hiyo ya kimuqawama imetekelezwa ndani ya kituo cha mafuta katika kitongoji hicho tajwa; ambapo kijana huyo wa Kipalestina aliondoka kwa gari katika eneo la tukio baada ya kutekeleza oparesheni hiyo. Nao wanajeshi wa Kizayuni walimmiminia risasi kijana huyo mwanamuqawama wakati akitoka ndani ya gari.  

Televisheni ya al Jazeera imetangaza kuwa hali ya kijana huyo wa Kipalestina aliyetekeleza oparesheni hiyo iliyowaangamiza Wazayuni wawili ni mbaya. Wakati huo huo vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa kijana mwingine wa Kipalestina amemjeruhi vibaya mlowezi mwingine wa Kizayuni karibu na mnara wa ulinzi wa Israel na kisha wanajeshi wa utawala huo wakamfyatulia risasi kijana huyo Mpalestina.  

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, helikopta ya jeshi la Israel ilitua katika eneo palipotekelezwa oparesheni dhidi ya Wazayuni katika kitongoji cha Ariel. 

342/