Ayatollah Nouri Hamedani amesisitiza kuwa kanuni za “Heshima, Hekima na Maslahi” pamoja na miongozo iliyowekwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu lazima zifuatwe kwa umakini, akibainisha kuwa viongozi wa serikali wana jukumu la kutekeleza sera kuu za taifa zilizoainishwa na uongozi wa juu wa nchi.
Marjaa wa Kidini Ayatollah Hussein Nouri Hamedani amesema kuwa kulinda umoja wa kitaifa na kuzuia migawanyiko ni kipaumbele cha juu kwa Iran, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha huduma kwa wananchi, kujibu ipasavyo uchokozi wa adui na kuendeleza nafasi ya mji wa Qom kama kitovu muhimu cha Kiislamu.