Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Mexico, Abolfazl Besandideh, amesema Fidel Castro hakuwa tu kiongozi wa kisiasa wa Cuba, bali aligeuka kuwa alama ya kimataifa ya mapambano ya watu wanaotetea uhuru, mamlaka ya kitaifa na kujitawala bila kuingiliwa na nguvu za nje.
Rais wa Cuba ametoa wito kwa mataifa ya Amerika ya Kusini kuimarisha umoja wao kufuatia operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyosababisha kukamatwa kwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, akitaja hatua hiyo kuwa ni “shambulio la kinyama” dhidi ya taifa huru.