Jana, Benjamin Netanyahu, Gideon Sa’ar Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni, pamoja na Abdirahman Mohamed Abdullahi, rais wa kujitangaza wa Somaliland, walitia saini tamko la pamoja la kuitambua Somaliland kama nchi huru na inayojitegemea.
Katika kipindi cha siku 50 za mapambano ya kistratejia baharini, harakati ya Ansarullah ya Yemen imeweza kusimama imara dhidi ya mashinikizo ya kijeshi na kisiasa ya Marekani na washirika wake, na hatimaye kuwadhihirishia ulimwengu kwamba dhamira ya mataifa huru inaweza kuvunja nguvu za mabeberu.