ICE

  • Maandamano Yatikisa Marekani, Minneapolis Kituo Kikuu cha Upinzani Dhidi ya ICE

    Maandamano Yatikisa Marekani, Minneapolis Kituo Kikuu cha Upinzani Dhidi ya ICE

    Wimbi la maandamano linaendelea kuitikisa Marekani, huku jiji la Minneapolis likiwa miongoni mwa vituo vikuu vya upinzani dhidi ya operesheni za polisi wa uhamiaji (ICE). Maelfu ya raia wameingia mitaani wakipinga matumizi ya nguvu kupita kiasi, na maandamano yamesambaa hadi miji mingine kama Portland, Maine, San Francisco na Washington DC. Serikali iko chini ya shinikizo kubwa la ndani, huku wananchi wakidai haki, uwazi na kuheshimiwa kwa utu wa raia.