Lapid

  • Lapid: Marekani iitaje Qatar kuwa “nchi adui”

    Lapid: Marekani iitaje Qatar kuwa “nchi adui”

    Kiongozi wa upinzani wa utawala wa Kizayuni, Yair Lapid, ameutaka utawala wa United States kuitangaza Qatar kuwa “nchi adui”. Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa mashirika makubwa ya Kiyahudi nchini Marekani, Lapid alidai kuwa uwekezaji wa kifedha wa Qatar katika vyuo vikuu vya Marekani unachochea kuenea kwa chuki dhidi ya Wayahudi na misimamo mikali. Aidha, alibainisha kuwa amewasilisha pendekezo la kuitambua Qatar kama nchi adui kisheria, akisisitiza kuwa taifa hilo ni “adui wa Marekani, Israeli na dunia.”