Ghadir Khum ni tukio la kihistoria lenye uzito mkubwa kwa Waislamu, hasa kwa wale wanaotilia mkazo nafasi ya Ahlul Bayt (a.s) katika uongozi wa umma. Ni siku ya kutafakari juu ya uongozi wa haki, kutambua mafundisho ya Mtume (s.a.w.w), na kuhuisha uhusiano wa kidini kwa msingi wa upendo, uadilifu, na utiifu kwa uongozi wa kweli wa Kiislamu.
Lengo la Mazungumzo Haya ni: Kuleta maelewano baina ya Madhehebu za Kiislamu na kuonyesha kuwa msingi wa Uimamu na Ukhalifa wa Maimam Kumi na Wawili wa Ahlul-Bayt (a.s), wanaofuatwa na Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, una mizizi pia katika vyanzo vinavyokubalika vya Kisunni.