Jarida la kihafidhina la Marekani The American Conservative limetoa onyo kwa Donald Trump, mgombea wa Urais wa Marekani mwaka 2024, likimtaka aepuke sera za kichochezi na vita, na badala yake aweke mkazo kwenye diplomasia kama njia bora ya kulinda maslahi ya Marekani.
Kwa mujibu wa jarida hilo, kuendelea na mwelekeo wa kijeshi na mivutano ya kimataifa hakutasaidia Marekani, bali kutazidisha matatizo ya kiuchumi na kisiasa, na kuathiri nafasi ya taifa hilo katika uongozi wa dunia.