Iran imewasilisha mapendekezo matatu ya kuimarisha ushirikiano wa vyuo vikuu, utafiti na teknolojia ndani ya Shirika la Ushirikiano wa Shanghai, huku ikisisitiza kuwa vyuo vikuu ni nguzo muhimu katika kujenga mustakabali wa jamii.
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran limetangaza mafanikio matatu makubwa ya nyuklia: kuzindua kichochezi cha kwanza cha viwandani kilichotengenezwa ndani ya nchi, kuanza uzalishaji wa hali ya juu wa Carbon-13, na kurejesha cyclotron kwa ajili ya uzalishaji wa dawa za mionzi licha ya vikwazo.