Mimi

  • Ni vipi Fatima Zahra (a.s) Alikuwa Mpenzi na Mpendwa Zaidi Katika Maisha ya Ali (a.s)?

    Ni vipi Fatima Zahra (a.s) Alikuwa Mpenzi na Mpendwa Zaidi Katika Maisha ya Ali (a.s)?

    Katika baadhi ya nyakati, mtu humtambulisha nafsi yake kwa kutaja nasaba yake na watu wakubwa. Hivyo ndivyo alivyofanya Amirul-Mu'minin Ali (a.s) katika mojawapo ya khutba zake baada ya kurejea kutoka vita vya Nahrawan. Ali (a.s) alisema: “Mimi ni mume wa Bibi Batul, Bibi wa wanawake wa ulimwengu, Fatima aliye mchamungu, msafi, mtukufu, mwongofu, mpendwa wa Mpenzi wa Allah, bora wa mabinti wake na mchanga wa roho ya Mtume wa Allah (s.a.w.).” Kutaja kwa Imam Ali (a.s) daraja la juu la Bibi Zahra (a.s) baada ya kujinasabisha na mwanamke huyu mtukufu ni kusisitiza nafasi kuu ya bibi huyu mbele ya mtu mkubwa kama Ali (a.s).