Oman
-
Mufti wa Oman:
“Inasikitisha kuwa waandishi wa habari wanauawa Gaza na baadhi wanaendelea kuwaunga mkono wavamizi”
Mufti wa Oman amelaani mauaji ya waandishi wa habari katika mji wa Gaza yaliyofanywa na jeshi la Israel, na kutamka masikitiko yake juu ya kuendelea kwa baadhi ya watu na nchi kuunga mkono wavamizi.
-
Ziara ya Pezeshkian nchini Oman | Mizinga 21 yafyatuliwa kwa heshima ya Rais wa Iran mjini Muscat
Dkt. Massoud Pezeshkian, Rais wa Iran, amefanya ziara nchini Oman kwa madhumuni ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kitamaduni. Alipowasili katika uwanja wa ndege wa Muscat, alipokelewa na maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo. Sherehe rasmi ya mapokezi ilifanyika katika Kasri ya Al-Alam kwa uwepo wa Sultan wa Oman, ambapo mizinga 21 ilifyatuliwa kwa heshima ya Rais wa Iran.
-
Raundi mpya ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani itafanyika Ijumaa hii Mjini Rome, Italia
Raundi ya tano ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani inatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa mjini Rome, Italia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza kuwa nchi yake imekubali pendekezo la Oman kwa ajili ya kikao hiki. Aidha, alisisitiza kuwa ujumbe wa Iran katika mazungumzo haya umejikita katika kulinda haki za taifa hilo na kuhakikisha kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran.