Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ali Khomeini katika mahojiano na mtandao wa habari wa Al-Mayadeen yaliyotangazwa Jumatano usiku, amesema anaiona mustakabali wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa mzuri, na kwamba njia pekee ya kuishi katika dunia ambayo Marekani na Israel wameigeuza kuwa msitu wa vurugu ni kupambana kwa msimamo (muqawama). Ameeleza kuwa Iran sasa iko katika vita vya kimaumbile ya uwepo wake.