Ziara ya siku ya Jumatano ya Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India, kwenda Israel, imezua ukosoaji mkubwa kutoka kwa vyama na makundi ya mrengo wa kushoto nchini humo.
Makundi hayo yamemshutumu kiongozi huyo wa kitaifa mwenye msimamo wa Uhindu kwa kushirikiana au kuunga mkono vita vinavyoendelea vya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Wakosoaji wanasema kuwa ziara hiyo inapingana na msimamo wa kihistoria wa India wa kuunga mkono haki za Wapalestina na suluhisho la mataifa mawili, na wameitaka serikali kutoa maelezo ya wazi kuhusu madhumuni ya safari hiyo pamoja na makubaliano yaliyofikiwa.