Balozi wa Iran nchini Iraq, Mohammad Kazem Al-Sadeq, amekutana na Patriarki (Baba-Kiongozi) mpya wa Kanisa la Kaldania, Mar Paulus III Nona, jijini Baghdad ambapo pande hizo zimesisitiza umuhimu wa kuimarisha maelewano ya kijamii, kuishi kwa amani kati ya dini mbalimbali na kuendeleza ushirikiano wa kikanda.
Katika kuendeleza diplomasia ya kidini na kuimarisha maadili ya kuishi kwa amani kati ya wafuasi wa dini mbalimbali, Rais wa Jamhuri alitoa ujumbe rasmi wa pongezi kwa kiongozi wa Wakatoliki duniani, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana, mazungumzo ya kidini na mshikamano wa kibinadamu katika dunia ya leo.