Waovu

  • Tamko la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

    Tamko la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

    Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) imesisitiza katika tamko lake kwamba: kuanzisha vita dhidi ya Iran ya Kiislamu ni sawa na kuvamia harem (makao matakatifu) ya Ahlul-Bayt (a.s). Katika hali hii, wanaharakati wote wa haki duniani, hasa mashirika na jumuiya zilizo chini ya mwavuli wa Ahlul-Bayt na wale wanaohusishwa na Jumuiya hii, wanaweza sasa kwa sauti kubwa kuliko wakati wowote kusema wazi kuwa utawala wa Kizayuni ni wa kigaidi na mvamizi. Aidha, taifa la Iran, likiwa limeungana zaidi na thabiti kuliko wakati wowote, litatoa jibu kali na la wazi kwa utawala huu wa kihalifu na muuaji wa watoto.