Dkt. Alwan alisema: Serikali ya Lebanon, kutokana na mipaka ya diplomasia na kutokuwepo kwa uimarishaji wa kweli wa jeshi (kwa sababu ya vizuizi vya Marekani), kimsingi haiwezi kuilinda nchi kijeshi.
Sheikh Ali Damuush amesema: “Kulegeza msimamo au kukubali mashinikizo na maagizo ya Marekani na Israel hakutaleta matokeo yoyote. Sisi hatutasalimu amri; hata ikiwa maadui wataweka juhudi zao zote kutuangamiza, kamwe hatutaacha njia ya muqawama (mapambano) wala kujitoa katika kuilinda nchi yetu.”