Marajii Wakuu wa Taqlid katika Ulimwengu wa Kishia, Ayatollah: Sistani, Makarem Shirazi, Nouri Hamedani, Javadi Amoli, Sobhani na Shabiri Zanjani wameshutumu katika taarifa tofauti matamshi ya udhalilishaji ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Dakta Hussein al-Moussawi amesema: Kufeli kwa fedheha kwa sera ya Netanyahu katika kupata ushindi wowote katika vita dhidi ya Ghaza, kushindwa kwake kudhibiti migogoro ya ndani na kujaribu kuukimbia utawala huo nje ya nchi ni sababu nyingine ya shambulio hilo dhidi ya Iran.