Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa ikieleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Pakistan na Afghanistan.
Iran imezitaka pande zote mbili kuanza mazungumzo ya haraka ili kusitisha mapigano, kuheshimu mamlaka na mipaka ya kila nchi, na kuepuka hatua zinazoweza kuongeza hali ya taharuki. Pia imetangaza utayari wake kusaidia juhudi za kupunguza mvutano na kufanikisha maelewano ya amani.