Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesisitiza kuwa makubaliano na Sultanate ya Oman ni sharti la lazima lakini halitoshi kwa ajili ya kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz ambao umekumbwa na matatizo tangu Machi 2026 kutokana na uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni, akibainisha kuwa Iran haifanyi mazungumzo yoyote na Marekani kwa sasa, na kwamba Pakistan ndiyo inayofanya kazi ya usuluhishi kati yao huku Qatar ikisaidia inapobidi.