Naibu Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, Liaqat Baloch, amesema Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) aliiongoza Iran kwa misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuifanya kuwa taifa la mapambano, huku akisisitiza umoja wa Umma wa Kiislamu na uungaji mkono wa kudumu kwa Palestina.
Gazeti la Yedioth Ahronoth linaripoti kuwa vita vya siku 12 dhidi ya Iran vilichukua mipango ya miaka miwili, na baadhi ya teknolojia za siri za Israel ziliharibika, ambapo kuibua upya kunahitaji miaka kadhaa na kuanza upya katika baadhi ya nyanja.