miongo mitano

  • Jumuiya ya Kiislamu Bangladesh: Waislamu Bilioni Mbili Wako Pamoja na Iran kwa Roho na Mali

    Jumuiya ya Kiislamu ya Bangladesh imetoa tamko rasmi ikitangaza uungaji mkono wake kamili kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kuonya kuwa shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran litakabiliwa na mwitikio mpana wa Waislamu duniani. Katika tamko hilo imesema: “Ingawa viongozi wa baadhi ya nchi za Kiislamu wanategemea Marekani na Israel, lakini Waislamu bilioni mbili duniani wamesimama pamoja na Palestina. Ikiwa uvamizi wa kijeshi utafanywa dhidi ya Iran, Waislamu kote duniani wataingia uwanjani kwa mali na nafsi zao; na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel utaanguka hivi karibuni.”