Katika ujumbe kuhusu kuaga kwa kishujaa kwa Kiongozi shahidi wa Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Mojtaba Khameni amesema kuwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Marekani wa makubaliano yaliyosainiwa kati ya marais wa Iran na Marekani umeonyesha tena kuwa saini ya rais wa Marekani haina thamani. Amesema pia kuwa Iran na mhimili wa muqawama wana masomo yasiyosahaulika kwa adui, kama ilivyoonekana kupitia ujasiri wa wapiganaji na uhodari wa wananchi wa maeneo ya kusini.