Katika Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu mjini Tehran, vitabu vitatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kazakhi vitazinduliwa rasmi, na miongoni mwao ni kitabu kiitwacho "Rafiki Yetu Mwenye Bahati", ambacho ni wasifu wa Shahidi Jenerali Qasem Soleimani.
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, pamoja na Waqfu mbalimbali alizotoa kwa Haram Tukufu ya Razavi katika zaidi ya miaka 40 iliyopita, ametoa waqfu wa vitabu vingi vya kale kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Haram Tukufu ya Razavi.