waondoke

  • Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq: Wavamizi wa Marekani Lazima Waondoke

    Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq: Wavamizi wa Marekani Lazima Waondoke

    Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq imesisitiza katika taarifa yake kwamba uwepo wa majeshi ya Marekani nchini Iraq ni aina ya uvamizi unaokiuka mamlaka ya taifa hilo, na imetaka kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutoka ardhi ya Iraq. “Wavamizi wanaendelea kukiuka anga la Iraq; iwe kupitia ndege zisizo na rubani (drones) au kwa kutumia ndege zao za kivita. Hatua hizi zinachukuliwa kuwa tishio kubwa kwa usalama, uthabiti na umoja wa ardhi ya nchi, na ni uvamizi wa wazi dhidi ya mamlaka na heshima ya dola ya Iraq.”