watawala

  • Onyo Kuhusu Mradi wa "Kuisahau Palestina" – Njama ya Kimataifa kwa Ushirikiano wa Viongozi wa Kiarabu

    Onyo Kuhusu Mradi wa "Kuisahau Palestina" – Njama ya Kimataifa kwa Ushirikiano wa Viongozi wa Kiarabu

    Kiongozi wa Harakati ya Kuamsha Ummah wa al-Mustafa: Kusahau Kadhia ya Palestina ni Njama Hatari na Usaliti Usiosameheka. Kiongozi wa Harakati ya Kuamsha Ummah wa Mustafa, katika hotuba yake ya hivi karibuni mjini Lahore, amekosoa vikali ukimya wa ulimwengu wa Kiislamu mbele ya uhalifu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina. Amesema kuwa kusahaulika kwa suala la Palestina ni njama hatari na usaliti usiosameheka, na akasisitiza kwamba ukimya huu – kuanzia vyombo vya habari hadi baadhi ya Serikali za Kiarabu – ni sehemu ya mradi wa kufuta kwa taratibu Palestina kutoka kwenye kumbukumbu ya Ummah wa Kiislamu.