Zana hizo zilitambulishwa wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Mkuu wa IRCG Meja Jenerali Hossein Salami, Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la IRGC, Admeli Alireza Tangsiri, na maafisa wengine wakuu wa serikali na kijeshi katika mji wa bandari wa Bandar Abbas, kusini mwa Iran jana Aklhamisi.
Manowari ya Shahidi Rais Ali Delvari, imepewa jina la shujaa mkuu wa taifa na mpigania uhuru aliyeongoza mapambano dhidi ya ukoloni kusini mwa Iran. Delvari, ambaye alipanga upinzani wa wananchi dhidi ya wanajeshi wa Uingereza, aliuawa shahidi mwaka 1915 akiwa na umri wa miaka 33, katika mapambano makali na wavamizi wa Uingereza katika mji wa bandari wa Bushehr, kusini mwa Iran.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la IRGC, Admeli Alireza Tangsiri alisema meli hiyo mpya ya kivita ya Iran inaweza kubeba meli tatu za kurusha makombora na helikopta ndani yake. Inaweza kushehenezwa na makombora yenye kupiga shabaha ya masafa ya kilomita 750, ameongeza.Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Kamanda Mkuu wa Jeshi la IRGC, Meja Jenerali Hossein Salami alisema vitengo vya wanamaji vya kikosi hicho vimepanua na kuimarisha uwezo wao kwa kiasi kikubwa.
Wakati huo huo, Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Iran kimepokea aina tofauti za mitambo na ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa ndani ya nchi wakati wa hafla iliyofanyika jana Alkhamisi. Msururu wa magari ya deraya yenye uzito wa kati na yale mazito kupita kiasi yamejumuishwa katika sekta ya ulinzi ya Jeshi la Ardhini, ikijumuisha magari ya mizinga na yale ya kivita.
342/
