Sisitizo hilo limetolewa katika kikao cha kamisheni kuu ya pamoja ya Iran na Malaysia kilichofanyika hapa mjini Tehran.
Katika kikao cha Kamisheni Kuu ya Pamoja ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Malaysia, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Malaysia walijadili na kubadilishana maoni kuhusiana na nyanja mbalimbali za uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za pande mbili na za pande kadhaa na pia katika majukwaa ya kieneo na kimataifa.
Seyyed Abbas Araghchi na Mohammad Hassan wamesisitiza azma ya viongozi wa nchi hizo mbili ya kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ili kuboresha zaidi uhusiano hususan katika nyanja za kiuchumi, kibiashara, kisayansi, kiteknolojia, kiutamaduni na kitaaluma.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiashiria utendaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupanua uhusiano na nchi za Asia na nchi zinazoendelea na za Kiislamu amesisitiza kwamba, Iran inatoa kipaumbele maalumu cha kustawisha uhusiano na Malaysia ikiwa miongoni mwa nchi muhimu katika bara la Asia na ulimwengu wa Kiislamu.
Araghchi amesifu na kupongeza misimamo yenye thamani na heshima ya serikali na watu wa Malaysia katika kuunga mkono haki halali za wananchi wa Palestina katika kipindi cha miezi kumi na sita ya mauaji ya kimbari na jinai za kivita zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
342/
