28 Februari 2025 - 17:35
Israel yakiri rasmi kushindwa katika oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa

Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa, katika mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka 2023 lilishindwa kuwahami walowezi wa utawala huo wanaoishi katika maeneo jirani na Gaza; na kwamba lilifeli katika masaa ya awali mkabala wa mashambulizi ya Hamas.

Jeshi la utawala wa kizayuni limetangaza katika taarifa yake kuwa hatua zilizopigwa katika vita vya karibuni haziwezi kuficha namna jeshi hilo lilivyoshindwa na kufeli mnamo Oktoba 7 mwaka 2023.

Jeshila utawala wa Kizayuni limetangaza kuwa idadi ya wanajeshi wao waliojeruhiwa na kuuawa na hasara walizopata ni kubwa ikilinganishwa na makadirio ya awali; na uchunguzi wa kiitelijinsia unaonyesha kuwa tathmini za Israeli zinatofautiana sana na hali halisi ya mambo maidanini.

Jeshi la utawala wa Israel limeongeza kuwa, taasisi za usalama wa utawala huo zilifeli kikamilifu usiku wa Oktoba 7 mwaka 2023, na wapinagaji wa Hamas huku wakitumia parachuti walifanikiwa kushambulia kambi na maeneo ya kijeshi ya Israel katika maeneo karibu na Gaza; katika hali ambayo makamanda wa jeshi la Israel walishindwa kutabiri kuhusu senario kama hiyo.

Si haya tu, bali jeshi la Israel limekiri kuwa kikosi cha anga cha utawala huo hakikuwa kimeandaa mpangowa dharura wa kukabiliana na tukio kama hilo na hatua ya wanamuqawama 5,600 wa Hamas ya kuingia kwa awamu tatu mtawalia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) iliushangaza sana utawala wa Kizayuni.

342/