28 Februari 2025 - 17:36
Afrika Kusini, Malaysia na Colombia zapinga meli zenye silaha katika bandari zao kwa ajili ya Israel

Viongozi wa Afrika Kusini, Malaysia na Colombia wametangaza katika jarida moja katika makala yao ya pamoja kwamba watazizuia meli zilizobeba silaha katika bandari za nchi hizo kwa ajili ya Israel.

Rais Cyril Paramphosa wa Afrika Kusini, Anwar Ibrahim Waziri Mkuu wa Malaysia na Rais Gustavo Petro wa Colombia katika makala yao ya pamoja katika Jarida la Foreign Policy wametaka kuhitimishwa kinga ya utawala wa Kizayuni katika kukiuka sheria za kimataifa.

Makala hiyo imeeleza kuwa: Chaguo liko wazi; imma kwa pamoja tuchukue hatua ili kutekeleza sheria za kimataifa la sivyo tutakuwa katika hatari ya kuporomoka.

Viongozi wa nchi hizo tatu pia wameeleza kuwa watazuia meli hizo zilizobeba silaha katiakbandari za nchi hiyo zenye lengo la kuuudhaminia silaha hizo utawala wa Israel;na watazuia usafirishaji wote wa silaha unaopelekea kukiukwa pakubwa sheria na kanuni za kibinadamu.

Ben Saul, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mapambano dhidi ya ugaidi alisema mwezi Januari kwamba Marekani na Ujerumani zinadhamini asilimia 99 ya silaha za utawala wa Kizayuni na kwamba hatua za kisheria dhidi ya nchi hizo zinapaswa kuchukuliwa.

342/